Hosted by Health Professionals Entrepreneurship and Mentorship
Programu hii imeandaliwa mahsusi kwa wataalamu wa afya waliopo kazini pamoja na wanafunzi wa kozi za afya wanaotaka kuandaliwa mapema kuunganisha taaluma ya afya na ujasiriamali. Lengo lake ni kuwajengea mtazamo sahihi (mindset), kuongeza uelewa wa fursa zilizopo ndani ya sekta ya afya, na kuwawezesha kubadili maarifa yao ya kitaaluma kuwa huduma au programu zinazoweza kulipiwa kwa njia halali, endelevu, na zinazozingatia maadili ya taaluma ya afya. Aidha, programu inawezesha washiriki kupata ujuzi wa matumizi bora ya mitandao ya kijamii kama nyenzo ya kitaaluma na kibiashara.
Kwa wanafunzi, programu husaidia kuanza kujipanga kitaaluma na kibiashara kabla ya kuhitimu, wakati kwa wataalamu waliopo kazini inalenga kupunguza utegemezi wa mshahara mmoja kwa kujenga utambulisho wa kitaaluma (personal/professional brand) na vyanzo vya ziada vya kipato. Hii ni mentorship ya vitendo inayolenga kuwaandaa wataalamu wa afya kwa mustakabali mpana zaidi unaovuka mipaka ya ajira ya kawaida.